Ni hali ya jicho kuwa jekundu kutokana na maambukizo kwenye jicho ya virusi au bakteria au matokeo ya aleji .
Dalili zake ni jicho kuwasha, kuwa jekundu, na kutoa majimaji na kuvimba.
Conjunctivitis inatibika kwa kutumia dawa kutokana na sababu iliyosababisha jicho kuwa jekundu. Dawa za kutibu conjuctivitis itokanayo na bakteria ni tofauti na dawa za kutibu conjuctivitis iliyosababishwa na virusi au aleji.